Kiswahili
Tume ya Lambeth katika Windsor Report “ilipendekeza na kuwahimiza viongozi wa majimbo kufikiria jinsi makanis ya Ushirika wa Kianglikana, yatakavyochukua na kufuatilia Agano sawa, ambalo litaonyesha waziwazi na kwa dhati, uaminifu, na ushikamano wa upendo, unaoendeleza uhusiano kati ya makanisa ya ushirika.[1]
IASCOME imejadili njia za kutekeleza sehemu muhimu za umisheni katika Ushirika wa Kianglikana kufuatia miaka kumi ya uijilisti na harakati ya Washirika Umusheni. Wazo la Agano Katika UMission lililzuka kuwa kipengele cha mbele. Twaamini ya kwamba Agano linaloshirikisha umuhimu wa umoja katika umisheni, lingeweza kuwa msingi wa husiano kati ya makanisa, mashirika ya umisheni na mitandao ya Ushirika huu zikatoa shabaha adhimu ya umoja katika umisheni kwa Ushirika wa Kianglikana (Anglican Communion).
Kwenye Maandiko, maagano ni muhimu hasa katika Agano La Kale kwa uhusano wa Mungu na Nuhu, Ibrahimu, Musa na uma wa Israeli. Jeremia na Ezekieli wanatabiri kuja kwa agano jipya- ambamo Mungu anawapa watu wake mioyo mipya na maisha mapya, naye atatembea nao, nao watatembea naye. Katika Agano Jipya, Yesu yuanzisha Agano hilo Jipya. Lilianzishwa na kuvunjwa kwa mwili wake na kumwagika kwa damu yake nalo lasherehekewa katika karamu muhimu ya Ushirika Utakatifu na kudhihirishwa kupitia Ufufuo wa Jesu Kristo kwa watu wote kwa nyakati zote.
IASCOME ilifikiria kwa undani Jinsi ya kubuni hulka ya agano. Tulitambua ya kwamba katika tamaduni zetu, agano ni makubaliano ya uzito na adhimu. Msingi wa maagano ni husiano ambamo watu hujitolea kwa hairi, hali mikataba yaweza kuwa mapatano ya kisheria chini ya Kanuni tawala. Maagano ni matoleo ya hairi mmoja kwa mwingine, hali mkataba unashikamanisha kwa utawala wa nje. Maagano ni ya kiuhusiano kati ya wanaofanya mapatano hayo na Kiuhusiano na Mungu na mbele ya Mungu.
Kwa vile sisi, Makanisa ya Kianglikana tuna desturi ya maagano yanayosaidia kufafanua uhusiano wetu na makanisa mengine, kwa mfano mapatano ya Porvoo kati ya Kanisa La Vingereza( Church of England) na makanisa ya Kilutheri eneo la bahari ya Baltic, na pia Wito kwa Umoja wa Umisheni, kati ya Kanisa la Episkopeli na Kanisa la uijilisti la kilutheri la Amerika.
Tunapendekeza kwa shauri ya ACC na majaribio ndani ya Ushirika, agano lifuatalo lenye vipengele tisa.Twaamini linatoa chanzo cha mapatano kati ya Makanisa ya Kianglikana kitaifa – bali pia yaweza kutumiwa katika parokia/makanisa, mashirika na mitandao ya umisheni, wenzi kati ya madiyosisi n.k. Twaamini Agano kwa Ushirika wa Kianglikana katika umisheni unatoa mwelekeo wa kushikamanisha huu ushirika pamoja kwa hali tofauti na ile ya ‘The Windsor Report’.
Agano Kwa Ushirika Katika Umisheni
Agano hili la bainisha umoja wa mwito wetu kushiriki katika Kazi ya Mungu ya uponyaji na upatanisho kwa ulimwengu wetu uliobarikiwa walakini hali ya kuvunjika na wenye maumivu.
Katika uhusiano wetu kama ndugu na dada wa Kianglikana dani ya Kristo, tunaamini katika tumaini la umoja ambalo Mungu ameleta kupitia Yesu katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Utangulizi huu unatambua ya kwamba, Ulimwengu ni mmoja ulioneemeshwa na Mungu lakini Kazi ya Mungu kupitia Kristo, inayofulizwa na roho Mtakatifu, ni ya kutafuta kuponya daumivu ya dunia na kupatanisha matengano. Utangulizi huu, watukumbusha ya kwamba sisi wakristo tumeitwa kushirikisha husiano zetu katika umisheni wa Mungu ulimwenguni, tukishuhudia ufalme wa upendo, haki na furaha ulioanzishwa na Yesu Mwenyewe.
Tukijengwa na Maadika na Sakramenti tunajitolea kwa:
Vipengele tisa via agano vimesimama katika maandiko na sakramenti panapopatikana chakula rohoni, wongozi na nguvu za safari kwa wenzi agano pamoja
Tunafnya Agano hili kwa ahadi ya jukumu letu kwa kila mmoja na kutegemeana kuliko ndani ya Mwili wa Kristo.
Mwisho huu watukumbusha ya kwamba tunahitajiana, tuna jukumu mmoja kwa mwingine na tunategemeana katika Mwili wa Kristo.
IASCOME inapendekeza ya kwamba ACC iweke Agano la Ushirika Katika Umisheni ya Ushirika wa Kianglikana waliotunukiwa kuendelea Kuangalia maagano kwa niaba ya Ushirika, kama ilivyopendekezwa na Windsor Report na “Communique” ya Februari 2005 ya mkutano wa viongozi. Kumaliza, IASCOME inatoa makubaliano haya kubainishwa na ACC-13:
MAAZIMIO YA ACC-
Hii kamati:
Agano limewakwa kwa ujumla makusudi. Katika kuelewa umisheni linajenga juu ya vipengele Vitano Vya Umisheni vya 1984 na 1990 Anglican consultative Council.[2] Linatoa muelekeo ambamo wanaoingia waweza kuona na kuchagua kazi na maelezo maalum yanayo fuatana na hali zao hususa.
[1] Windsor Report pp. 62-64
[2] Kutangaza habari vyema ya ufalme wa Mungu; kufunza, kubatiza na kulea waamini wapya; kutumika katika mahitaji ya kibinadamu, kutafuta kubadilisha hali zisizo haki katika jamii , kufanya bidii kulinda vyote alivyoviumba Mungu na kustawisha na kuboresha maisha ya dunia.